Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia al-Mughiyrah bin Shu´bah (Radhiya Allaahu ´anh) pindi alipotaka kumvua soksi zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ziache kwani hakika nilizivaa wakati nilipokuwa na twahara. Kisha akapangusa juu yake.”

Hakuna tofauti baina ya kwamba twahara hii alipangusa mguu au alipangusa soksi ilio chini yake. Kwa mfano lau mtu atatawadha wudhuu’ kikamilifu ikiwa ni pamoja na miguu. Baada ya hapo akavaa soksi. Katika hali hii anahesabika amezivaa akiwa na twahara.

Vilevile lau atakuwa amevaa soksi hapo kabla na akapangusa juu yake kisha akahitajikuongeza soksi zingine na akazivaa juu ya soksi zile za mwanzo ambazo alipangusa juu yake – ilihali bado ni mwenye twahara – apanguse juu ya zile za pili. Lakini hata hivyo ataanza kuhesabu muda tokea wakati pale alipoanza kupangusa zile za kwanza na sio tokea pale alipoanza kupangusa zile za pili. Haya ndio maoni sahihi. Akivaa soksi juu ya soksi alizotangulia kupangusa juu yake, apanguse juu ya zile zilizo juu. Lakini hata hivyo kuhusiana na muda ajengee tokea pale ambapo alianza kupangusa zile za kwanza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/111-112)
  • Imechapishwa: 08/02/2023