Swali: Watu wengi wanasema iwapo watu wawili tu wataswali pamoja, basi ni lazima yule maamuma aliye pembeni arudi nyuma kidogo?
Jibu: Hapana, wapange safu sawa. Imamu apange safu sawa na maamuma iwapo ni wawili. Lakini wakiwa ni watatu basi bora wale maamuma wawili wapange safu nyuma.
Swali: Wanajengea hoja kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliposema:
”Msilingane sawa na imamu na wala msimtangulie mbele.”
Jibu: Hapana, haina msingi. Walingane naye. Ni nani aliyesema wasilingane sawa naye? Sio Hadiyth.
Swali: …imamu katika Sujuud na Rukuu´?
Jibu: Ndio, asitanguliwe. Lakini hakuna inayosema kwamba msilingane naye sawa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24648/كيفية-استواء-الامام-والماموم-اذا-كانوا-اثنين
- Imechapishwa: 19/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)