Swali: Ni ipi namna ya kuandika mkataba wa ndoa? Anasema nini yule anayefungisha ndoa? Sisi mashahidi tunasoma nini ilihali hatukumuuliza msichana kama ameridhia au hakuridhia, bali tulitegemea maneno ya baba yake kwamba ameridhia?
Jibu: Sunnah ni kwamba mwenye kufungisha ndoa au walii au mume asome Khutbah ya haja. Hii ndiyo Sunnah:
“Himdi zote njema anastahiki Allaah, tunamhimidi Allaah, tunamuomba msaada na msamaha Wake. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na shari za nafsi zetu na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na anayempoteza, hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake.”
Kisha husoma Aayah tatu zinazojulikana.
Baada ya hapo anamwambia walii ”Sema: “Nimekuozesha binti yangu” au “dada yangu” au “binti wa ndugu yangu fulani.” Na mume anasema: “Nimekubali ndoa hii.”
Hapo ndoa inakuwa imekamilika.
Mashahidi wanasikiliza ili washuhudie yaliyotokea. Mashahidi wawili au zaidi hushuhudia kuwa fulani mwana wa fulani amemuoa fulani msichana wa fulani.
Ama kuhusu ridhaa ya msichana, hilo ni jukumu la mwenye kufungisha ndoa au hakimu. Yeye ndiye anayehakikisha kuwepo kwa ridhaa au kutokuwepo kwake, kwa kumuuliza walii au kwa njia nyingine zinazofaa.
Mashahidi wao hushuhudia tukio lililotokea tu kwamba ndoa imefanyika mbele yao, chini ya uangalizi wa mwenye kufungisha ndoa au hakimu. Hiyo inatosha.
Mwanafunzi: Kwa hiyo hawatoenda kuchukua kukubali kwake?
Ibn Baaz: Hapana, hilo ni kwa mfungisha ndoa. Yeye ndiye anayesimamia jambo hilo au hakimu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3328/ما-يقال-عند-عقد-النكاح-وبماذا-يشهد-الشهود
- Imechapishwa: 03/10/2026
Swali: Ni ipi namna ya kuandika mkataba wa ndoa? Anasema nini yule anayefungisha ndoa? Sisi mashahidi tunasoma nini ilihali hatukumuuliza msichana kama ameridhia au hakuridhia, bali tulitegemea maneno ya baba yake kwamba ameridhia?
Jibu: Sunnah ni kwamba mwenye kufungisha ndoa au walii au mume asome Khutbah ya haja. Hii ndiyo Sunnah:
“Himdi zote njema anastahiki Allaah, tunamhimidi Allaah, tunamuomba msaada na msamaha Wake. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na shari za nafsi zetu na maovu ya matendo yetu. Anayemuongoza Allaah, basi hakuna wa kumpoteza, na anayempoteza, hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia kuwa hapana anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake.”
Kisha husoma Aayah tatu zinazojulikana.
Baada ya hapo anamwambia walii ”Sema: “Nimekuozesha binti yangu” au “dada yangu” au “binti wa ndugu yangu fulani.” Na mume anasema: “Nimekubali ndoa hii.”
Hapo ndoa inakuwa imekamilika.
Mashahidi wanasikiliza ili washuhudie yaliyotokea. Mashahidi wawili au zaidi hushuhudia kuwa fulani mwana wa fulani amemuoa fulani msichana wa fulani.
Ama kuhusu ridhaa ya msichana, hilo ni jukumu la mwenye kufungisha ndoa au hakimu. Yeye ndiye anayehakikisha kuwepo kwa ridhaa au kutokuwepo kwake, kwa kumuuliza walii au kwa njia nyingine zinazofaa.
Mashahidi wao hushuhudia tukio lililotokea tu kwamba ndoa imefanyika mbele yao, chini ya uangalizi wa mwenye kufungisha ndoa au hakimu. Hiyo inatosha.
Mwanafunzi: Kwa hiyo hawatoenda kuchukua kukubali kwake?
Ibn Baaz: Hapana, hilo ni kwa mfungisha ndoa. Yeye ndiye anayesimamia jambo hilo au hakimu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3328/ما-يقال-عند-عقد-النكاح-وبماذا-يشهد-الشهود
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/namna-inavyofungwa-ndoa-katika-uislamu/