Swali: Mmoja wa ndugu amekuja na nakala ya msahafu iliyochapishwa Pakistan na ndani yake katika du´aa ya kumaliza Qur-aan kuna maneno kama: “Utunusuru dhidi ya watu makafiri kwa heshima ya Qur-aan hii Tukufu” na pia “Pamba tabia zetu kwa hadhi ya Qur-aan Tukufu” na “Tufanyie wepesi maumivu ya kifo kwa hadhi ya Qur-aan Tukufu.” Unasemaje juu ya haya?
Jibu: Du´aa hii na aina hii ya Tawassul haijulikani kutoka kwa Salaf. Hapana shaka kuwa Qur-aan ina heshima na daraja kubwa. Lakini maneno kama ´kwa hadhi ya Qur-aan Tukufu` ni maneno ya wajinga. Qur-aan ni maneno ya Allaah. Hivyo Tawassul kwa majina ya Allaah na sifa Zake ni haki na ni sababu ya kujibiwa du´aa. Ikiwa mtu atasema:
”Ee Allaah! Nakuomba kwa kuithamini kwangu Qur-aan”, “kwa kufuata kwangu Qur-aan” au “kwa kushikamana kwangu na njia ya Qur-aan” basi hiyo ni njia nzuri. Aidha akisema “kwa Qur-aan Tukufu”, basi hiyo inaweza kuwa ni kufanya Tawassul kwa sifa za Allaah, kwa sababu Qur-aan ni maneno Yake. Ama matamshi yaliyotajwa hapo juu hayana maana sahihi. Ni maneno yasiyo ya kisomi yasiyo na msingi.
Hivyo linalofaa ni mtu kufanya Tawassul kwa uwazi kwa majina ya Allaah na sifa Zake, kama alivosema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
”Allaah ana Majina mazuri kabisa, hivyo basi muombeni kwayo.”[1]
Akisema ”Ee Allaah! Nisamehe kwa rehema Zako, ee Mwenye kurehemu zaidi”, “Nisamehe kwa sababu ya kufuata kwangu Kitabu Chako Tukufu”, “kwa kushikamana kwangu na njia Yake”, ”Hakika Wewe ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu” na mfano wa hayo katika Tawassul iliyo sahihi kwa majina na sifa Zake (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1] 07:180
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3320/حكم-قول-القاىل-بجاه-القران-الكريم
- Imechapishwa: 03/10/2026
Swali: Mmoja wa ndugu amekuja na nakala ya msahafu iliyochapishwa Pakistan na ndani yake katika du´aa ya kumaliza Qur-aan kuna maneno kama: “Utunusuru dhidi ya watu makafiri kwa heshima ya Qur-aan hii Tukufu” na pia “Pamba tabia zetu kwa hadhi ya Qur-aan Tukufu” na “Tufanyie wepesi maumivu ya kifo kwa hadhi ya Qur-aan Tukufu.” Unasemaje juu ya haya?
Jibu: Du´aa hii na aina hii ya Tawassul haijulikani kutoka kwa Salaf. Hapana shaka kuwa Qur-aan ina heshima na daraja kubwa. Lakini maneno kama ´kwa hadhi ya Qur-aan Tukufu` ni maneno ya wajinga. Qur-aan ni maneno ya Allaah. Hivyo Tawassul kwa majina ya Allaah na sifa Zake ni haki na ni sababu ya kujibiwa du´aa. Ikiwa mtu atasema:
”Ee Allaah! Nakuomba kwa kuithamini kwangu Qur-aan”, “kwa kufuata kwangu Qur-aan” au “kwa kushikamana kwangu na njia ya Qur-aan” basi hiyo ni njia nzuri. Aidha akisema “kwa Qur-aan Tukufu”, basi hiyo inaweza kuwa ni kufanya Tawassul kwa sifa za Allaah, kwa sababu Qur-aan ni maneno Yake. Ama matamshi yaliyotajwa hapo juu hayana maana sahihi. Ni maneno yasiyo ya kisomi yasiyo na msingi.
Hivyo linalofaa ni mtu kufanya Tawassul kwa uwazi kwa majina ya Allaah na sifa Zake, kama alivosema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا
”Allaah ana Majina mazuri kabisa, hivyo basi muombeni kwayo.”[1]
Akisema ”Ee Allaah! Nisamehe kwa rehema Zako, ee Mwenye kurehemu zaidi”, “Nisamehe kwa sababu ya kufuata kwangu Kitabu Chako Tukufu”, “kwa kushikamana kwangu na njia Yake”, ”Hakika Wewe ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu” na mfano wa hayo katika Tawassul iliyo sahihi kwa majina na sifa Zake (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1] 07:180
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3320/حكم-قول-القاىل-بجاه-القران-الكريم
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/kuomba-duaa-kwa-jaha-na-hadhi-ya-qur-aan-tukufu/