Hedhi humzuia mwanamke mambo kumi:
1 – Kuswali.
2 – Uwajibu wa swalah.
3 – Kufunga.
4 – Kutufu.
5 – Kusoma Qur-aan.
5 – Kugusa msahafu.
7 – Kukaa msikitini.
8 – Kufanya jimaa kwenye tupu.
9 – Kutoa talaka.
10 – Kuhesabu eda kwa miezi.
Hedhi inapelekea ulazima wa josho la janaba, kufikia baleghe na kuanza eda kutokana nayo.
Damu inapokatika, basi inajuzu kufunga na kutoa talaka. Lakini mambo mengine yaliyotajwa hayaruhusiwi mpaka aoge josho la janaba.
Inajuzu kustarehe na mwanamke mwenye hedhi kwa kisichokuwa kitendo cha ndoa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Fanyeni kila kitu isipokuwa jimaa.”[1]
Kiwango cha chini cha hedhi ni siku moja na usiku wake. Kiwango chake cha juu ni siku kumi na tano. Kiwango cha chini cha twahara baina ya hedhi mbili ni siku kumi na tatu, lakini hakuna kiwango cha juu chake. Umri wa chini ambao mwanamke anaweza kupata hedhi ni miaka tisa na kiwango chake cha juu ni miaka sitini.
Mwanamke anayeanza kupata hedhi yake ya kwanza, atajizuia na ´ibaadah akiona damu katika wakati ambao kwa kawaida mwanamke hupata hedhi. Ikiwa damu itakatika kabla ya kutimia siku moja na usiku wake, basi si hedhi. Ikiwa itazidi hapo na asivuke kiwango cha juu cha hedhi, basi hiyo ni hedhi. Ikiwa hali hiyo itajirudia kwa miezi mitatu kwa namna ileile, huwa ni ada yake ya mwezi.
Ikiwa damu itazidi kiwango hicho, basi ziada yake ni damu ya ugonjwa. Katika hali hiyo ni juu yake kuoga wakati hedhi itakapomalizika, kuosha tupu yake, kuzuia damu kutoka na kutawadha wakati wa kila swalah, kisha aswali. Hukumu hiyohiyo inamuhusu yule ambaye mkojo unamtoka bila kukatika na mwenye hali mfano wa hiyo.
Ikiwa damu itaendelea kwake katika mwezi unaofuata, basi ikiwa alikuwa na ada ya mwezi, hedhi yake ni siku za ada yake. Na ikiwa hakuwa na ada ya mwezi lakini ana uwezo wa kutofautisha damu – kwa namna ya kwamba baadhi ya damu yake ni nyeusi na nzito, na nyingine ni nyekundu na nyepesi – basi hedhi yake ni katika kipindi cha damu nyeusi na nzito. Ikiwa ni mwanamke anayeanza kupata hedhi, amesahau ada yake ya mwezi, au hana uwezo wa kutofautisha damu, basi hedhi yake katika kila mwezi ni siku sita au saba. Kwa sababu huo ndio wakati ambao kwa kawaida wanawake wengi hupata hedhi.
Mwanamke mjamzito hapati hedhi, isipokuwa akiona damu siku moja au mbili kabla ya kujifungua, basi hiyo ni damu ya uzazi.
[1] Muslim (301).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 18-19
- Imechapishwa: 03/10/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 18-19
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/10-damu-ya-hedhi/