Namna yake ni kupiga mikono yake juu ya ardhi safi pigo moja. Kisha apanguse kwa mikono hiyo uso wake na viganja vyake. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Ammaar:
“Ilikuwa inakutosheleza kufanya namna hii.” Kisha akapiga mikono yake juu ya ardhi na akapaka kwa hiyo uso na viganja vyake.”[1]
Inajuzu ikiwa atafanya Tayammum kwa mapigo zaidi ya moja au akapaka sehemu zaidi.
Kujitwaharisha kwa udongo kuna masharti manne:
1 – Kushindwa kutumia maji, ima kwa kutokuwepo kwake, kuogopa madhara kwa kuyatumia kwa sababu ya maradhi, baridi kali, kuogopa kiu juu yake mwenyewe, mwenzake au mnyama wake. Hukumu ni hiyohiyo ikiwa ataogopa juu yake mwenyewe au mali yake katika kuyatafuta au kutopatikana kwake isipokuwa kwa bei kubwa. Ikiwa anaweza kuyatumia katika baadhi ya mwili wake au akapata maji yasiyotosha kwa twahara yake, basi atayatumia na atafanya Tayammum kwa viungo vingine vilivyobaki.
2 – Wakati. Hafanyi Tayammum kwa ajili ya swalah ya faradhi kabla ya kuingia wakati wake wala kwa ajili ya swalah ya Sunnah katika wakati ambao imekatazwa kuiswali.
3 – Nia. Ikiwa atafanya Tayammum kwa ajili ya swalah ya Sunnah, basi haswali kwa Tayammum hiyo swalah ya faradhi. Ikiwa atafanya Tayammum kwa ajili ya swalah ya faradhi, basi anaweza kuitekeleza na kutekeleza atakavyo katika swalah za faradhi na swalah za Sunnah mpaka wakati wake utoke.
4 – Udongo. Hafanyi Tayammum isipokuwa kwa udongo msafi wenye vumbi.
Tayammum huchenguka kwa yaleyale yanayochengua twahara ya maji, na kutoka kwa wakati na kuweza kutumia maji – hata ikiwa yuko ndani ya swalah.
[1] al-Bukhaariy (338) na Muslim (340 na 368).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 17-18
- Imechapishwa: 03/10/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 17-18
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/09-tayammum/