Ni lazima kuoga josho la janaba baada ya kutokwa na manii, nayo ni maji yanayotoka kwa msukumo na kukutana kwa sehemu mbili za tohara.
Ni wajibu katika kuoga josho la janaba kutia nia, kuosha mwili wake wote pamoja na kusukutua na kuvuta maji puani.
Wakati wa uogaji ni wajibu kuanza na kutaja jina la Allaah, kusugua mwili wake kwa mikono yake na afanye kama alivyosimulia Maymuunah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
”Nilimfunika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha akaoga janaba. Akaanza kwa kuosha mikono yake, kisha akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, akaosha tupu yake na sehemu zilizopatwa na hayo, kisha akaupiga mkono wake ukutani na ardhini, kisha akatawadha kama anavyotawadha kwa ajili ya swalah, kisha akamimina maji juu ya mwili wake wote, kisha akasogea na akaosha miguu yake.”[1]
Si lazima kufungua nywele katika kuoga josho la janaba ikiwa maji yamefika kwenye mashina yake.
Ikiwa kwa kuoga kwake josho la janaba atanuia twahara mbili, itamtosheleza kwa zote mbili. Kadhalika ikiwa atafanya Tayammum kwa hadathi mbili na najisi ikiwa kwenye mwili wake, itamtosheleza kwa zote. Ikiwa atanuia najisi moja wapo, basi hatapata isipokuwa kile alichonuia.
[1] al-Bukhaariy (249) na Muslim (317).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 17
- Imechapishwa: 03/10/2026
Ni lazima kuoga josho la janaba baada ya kutokwa na manii, nayo ni maji yanayotoka kwa msukumo na kukutana kwa sehemu mbili za tohara.
Ni wajibu katika kuoga josho la janaba kutia nia, kuosha mwili wake wote pamoja na kusukutua na kuvuta maji puani.
Wakati wa uogaji ni wajibu kuanza na kutaja jina la Allaah, kusugua mwili wake kwa mikono yake na afanye kama alivyosimulia Maymuunah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
”Nilimfunika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha akaoga janaba. Akaanza kwa kuosha mikono yake, kisha akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, akaosha tupu yake na sehemu zilizopatwa na hayo, kisha akaupiga mkono wake ukutani na ardhini, kisha akatawadha kama anavyotawadha kwa ajili ya swalah, kisha akamimina maji juu ya mwili wake wote, kisha akasogea na akaosha miguu yake.”[1]
Si lazima kufungua nywele katika kuoga josho la janaba ikiwa maji yamefika kwenye mashina yake.
Ikiwa kwa kuoga kwake josho la janaba atanuia twahara mbili, itamtosheleza kwa zote mbili. Kadhalika ikiwa atafanya Tayammum kwa hadathi mbili na najisi ikiwa kwenye mwili wake, itamtosheleza kwa zote. Ikiwa atanuia najisi moja wapo, basi hatapata isipokuwa kile alichonuia.
[1] al-Bukhaariy (249) na Muslim (317).
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 17
Imechapishwa: 03/10/2026
https://firqatunnajia.com/08-kuoga-baada-ya-josho-la-janaba/