Namna Hii Ndivyo Inavyotolewa Zakaah Kwa Ajili Ya Deni La Fakiri

Swali: Je, inafaa kwangu kulipa zakaah yangu kwa kulipa deni la fakiri moja kwa moja au nimpe pesa yeye kisha baadae atajilipia mwenyewe?

Jibu: Hili la pili. Mpe fakiri zakaah halafu yeye mwenyewe atazitumia kwa ajili ya mambo yake kama kulipa deni, matumizi na mengineyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017