Swali: Je, najisi ya wanyama wakali na kila mwenye meno ya kunyanyua ni kama najisi ya mbwa na nguruwe?
Jibu: Ndiyo, najisi yao ni najisi ya asili. Kwa maana kwamba viumbe vyao vyenyewe ni najisi. Lakini najisi ya mbwa ni kali zaidi. Kwa sababu hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mbwa akilamba chombo cha mmoja wenu, basi akioshe mara saba, ambapo mojawapo ikiwa kwa udongo.”
Hii ni maalum kwa kulamba kwa mbwa. Ama wanyama wengine wakali, najisi yao ni nyepesi zaidi, ingawa wao ni najisi. Kwa hiyo wanyama wote wakali ni najisi ya asili. Ama kuja kwao kwenye maji ni jambo jingine. Maji ambayo wanyama wakali wanayafikia, hukumu yake ya asili ni kuwa ni twahara, isipokuwa ikiwa yatabadilika. Vivyo hivyo punda wa kufugwa ni najisi ya asili. Lakini akinywa katika maji, basi hukumu ya asili ya maji hayo ni kuwa ni twahara.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
- Imechapishwa: 25/09/2026
Swali: Je, najisi ya wanyama wakali na kila mwenye meno ya kunyanyua ni kama najisi ya mbwa na nguruwe?
Jibu: Ndiyo, najisi yao ni najisi ya asili. Kwa maana kwamba viumbe vyao vyenyewe ni najisi. Lakini najisi ya mbwa ni kali zaidi. Kwa sababu hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mbwa akilamba chombo cha mmoja wenu, basi akioshe mara saba, ambapo mojawapo ikiwa kwa udongo.”
Hii ni maalum kwa kulamba kwa mbwa. Ama wanyama wengine wakali, najisi yao ni nyepesi zaidi, ingawa wao ni najisi. Kwa hiyo wanyama wote wakali ni najisi ya asili. Ama kuja kwao kwenye maji ni jambo jingine. Maji ambayo wanyama wakali wanayafikia, hukumu yake ya asili ni kuwa ni twahara, isipokuwa ikiwa yatabadilika. Vivyo hivyo punda wa kufugwa ni najisi ya asili. Lakini akinywa katika maji, basi hukumu ya asili ya maji hayo ni kuwa ni twahara.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
Imechapishwa: 25/09/2026
https://firqatunnajia.com/najisi-ya-wanyama-wakali-na-mwenye-meno-ya-kunyanyua/