Mzee anayeng´ang´ania kufunga ilihali funga inamdhuru

hivyo anaendelea kufunga pamoja na kuwa hilo linadhuru afya yake. Je, kuna kafara kwa kutokufunga kwake na ni ipi?

Jibu: Ikiwa kufunga kunadhuru afya yake basi  haijuzu kwake kufunga. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا

“Msizijue nafsi zenu. Kwani Allaah kwenu ni Mwenye kurehemu.” (04:29)

وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ

“Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.” (02:195)

Kwa hivyo haijuzu kwake kufunga ilihali swawm inadhuru afya yake. Maadamu ameshakuwa na umri mkubwa basi mara nyingi ni kuwa hawezi kufunga huko mbeleni. Hivyo basi, anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini. Ima awape chakula masikini ambapo kiwango chake ni robo pishi ya ngano au nusu pishi ya kitu kingine. Mchele ni kama ngano kwa kuwa watu wanavyonufaika nao ni kama wanavyonufaika na ngano. Bali mchele una manufaa zaidi kwa kuwa hauna ugumu kama ilivyo inapokua kwa ngano au vilevile anaweza kupika chakula na akawaalika masikini kutokana na ile idadi ya masiku anayodaiwa kwa mwezi. Hivyo ndivyo itatakasika dhimma yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/123-124)
  • Imechapishwa: 19/06/2017