Swali: Vipi ikiwa mwanamke ataona mwezi mwandamo?

Jibu: Kuna tofauti za maono juu ya suala hili. Lakini kauli iliyo wazi zaidi ni kwamba ushahidi wake hautoshi. Hii ni kwa sababu masuala haya ni makubwa na ya kidini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwategemea wanaume katika ushahidi wa kuuona mwezi, kama inavyodhihirika katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas kuhusu mbedui na Hadiyth ya Ibn ´Umar.

Swali: Ikiwa mtu atasema kwamba ushahidi wa mwanamke unakubalika kwa mujibu wa mlango wa upokezi wa Hadiyth?

Jibu: Hili ni jambo tofauti, kwa sababu upokezi wa Hadiyth si sawa na kuthibitisha wakati wa ´ibaadah. Inapokuja katika upokezi wa Hadiyth ushahidi wa mwanamke unakubalika.

Swali: Je, inakubalika kuangalia mwezi kwa kutumia darubini?

Jibu: Ikiwa mtu atauona mwezi kwa macho yake moja kwa moja, haijalishi kitu ni kwa msaada wa darubini au bila, basi ushahidi wake unakubalika.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25430/حكم-روية-المراة-الهلال-وحكم-الروية-بالمجهر
  • Imechapishwa: 01/04/2025