Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri basi humpa ufahamu akaielewa dini.”[1]
Hadiyth hii ni miongoni mwa fadhilah kubwa kabisa za elimu na kwamba elimu yenye manufaa ni moja ya alama za furaha ya mja na kwamba Allaah anamtakia kheri.
Kuwa na uelewa katika dini kunakusanya kuwa na uelewa katika misingi ya imani, Shari´ah na hukumu za Uislamu na hakika za Ihsaan. Kwani dini imekusanya mambo yote mtatu, kama ilivyo katika Hadiyth ya Jibriyl wakati alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Uislamu, imani na Ihsaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamjibu swali lake na akamfasiria imani kwa misingi yake sita, Uislamu kwa nguzo zake tano na akafasiri Ihsaan kwamba:
“Ni kumwabudu Allaah kama vile unamuona. Ikiwa humuoni basi tambua kuwa Yeye anakuona.”[2]
Uelewa kusudiwa kunaingia vilevile kuwa na uelewa katika ´Aqiydah na kuwa na utambuzi juu ya mfumo wa Salaf na kuyatendea kazi kwa nje na kwa undani. Sambamba na hilo mtu awe na utambuzi juu ya madhehebu ya wale wenye kwenda kinyume na kubainisa makosa yao kutokamana na Qur-aan na Sunnah – yote yanaingia katika kuwa na uelewa.
[1] al-Bukhaariy (71) na Muslim (1037).
[2] Muslim (8).
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bahjatu Quluub-il-Abraar, uk. 33
- Imechapishwa: 24/01/2019
Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule ambaye Allaah anamtakia kheri basi humpa ufahamu akaielewa dini.”[1]
Hadiyth hii ni miongoni mwa fadhilah kubwa kabisa za elimu na kwamba elimu yenye manufaa ni moja ya alama za furaha ya mja na kwamba Allaah anamtakia kheri.
Kuwa na uelewa katika dini kunakusanya kuwa na uelewa katika misingi ya imani, Shari´ah na hukumu za Uislamu na hakika za Ihsaan. Kwani dini imekusanya mambo yote mtatu, kama ilivyo katika Hadiyth ya Jibriyl wakati alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Uislamu, imani na Ihsaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamjibu swali lake na akamfasiria imani kwa misingi yake sita, Uislamu kwa nguzo zake tano na akafasiri Ihsaan kwamba:
“Ni kumwabudu Allaah kama vile unamuona. Ikiwa humuoni basi tambua kuwa Yeye anakuona.”[2]
Uelewa kusudiwa kunaingia vilevile kuwa na uelewa katika ´Aqiydah na kuwa na utambuzi juu ya mfumo wa Salaf na kuyatendea kazi kwa nje na kwa undani. Sambamba na hilo mtu awe na utambuzi juu ya madhehebu ya wale wenye kwenda kinyume na kubainisa makosa yao kutokamana na Qur-aan na Sunnah – yote yanaingia katika kuwa na uelewa.
[1] al-Bukhaariy (71) na Muslim (1037).
[2] Muslim (8).
Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Bahjatu Quluub-il-Abraar, uk. 33
Imechapishwa: 24/01/2019
https://firqatunnajia.com/mwenye-uelewa-anawafuata-salaf-na-anawaraddi-ahl-ul-bidah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)