Mwenye kumtolea swadaqah aliyechelewa wakati uliokatazwa

Swali: Kuna mtu amepitwa na swalah ya Fajr au ´Aswr pamoja na mkusanyiko akaingia msikitini – je, nimpe swadaqah kwa kuswali pamoja naye japokuwa ni wakati uliokatazwa kuswali ndani yake? Je, mimi niwe imamu au maamuma wake?

Jibu: Hapana neno. Imekuja katika Hadiyth:

“Ni nani atakayempa swadaqah huyu na akaswali pamoja naye?”

Ama kuswali katika wakati uliokatazwa katika hali hii ni jambo limevuliwa. Kwa sababu ni kwa sababu. Yale mambo yenye sababu yamevuliwa. Kwa mfano Tahiyyat-ul-Masjid, swalah ya jeneza, swalah ya kupatwa kwa jua na kuirudi swalah. Lau mtu ataswali ´Aswr kwenye msikiti fulani kisha akaenda kwenye msikiti mwingine ambapo kuna mzunguko wa kielimu akawakuta wanaswali ambapo akaswali pamoja nao kwa mara ya pili, inakuwa Naafilah. Ni mamoja ni swalah ya ´Aswr au Fajr. Kadhalika ikiwa atampa swadaqah mtu huyu kwa kuswali pamoja naye.

Bora zaidi yeye ndiye awe imamu. Hakuna neno vilevile ikiwa wewe utakuwa imamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (09) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191370#219699
  • Imechapishwa: 15/03/2019