Swali: Ikiwa mtu ameamka wakati wa alfajiri na muda wa swalah ya Fajr unakaribia kumalizika na yeye yuko katika hali ya janaba. Je, aswali akiwa katika janaba ili usimpite muda au aoge hata kama muda utatoka?
Jibu: Inamlazimu kuoga josho la janaba hata kama muda wa swalah utatoka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]
Kwa hiyo wakati wake ni wakati wa kuamka kwake. Anapoamka kutoka usingizini na kukumbuka, basi anaharakisha kuoga josho na kuswali. Hakuna tatizo lolote kwake, kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru.
[1]al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1050/اذا-ضاق-الوقت-على-الجنب-فهل-يتيمم-او-يغتسل
- Imechapishwa: 03/01/2026
Swali: Ikiwa mtu ameamka wakati wa alfajiri na muda wa swalah ya Fajr unakaribia kumalizika na yeye yuko katika hali ya janaba. Je, aswali akiwa katika janaba ili usimpite muda au aoge hata kama muda utatoka?
Jibu: Inamlazimu kuoga josho la janaba hata kama muda wa swalah utatoka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]
Kwa hiyo wakati wake ni wakati wa kuamka kwake. Anapoamka kutoka usingizini na kukumbuka, basi anaharakisha kuoga josho na kuswali. Hakuna tatizo lolote kwake, kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru.
[1]al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1050/اذا-ضاق-الوقت-على-الجنب-فهل-يتيمم-او-يغتسل
Imechapishwa: 03/01/2026
https://firqatunnajia.com/mwenye-janaba-anakhofia-akioga-utamalizika-wakati-wa-fajr/