Mwanaume kuziacha ndevu zake ni khiyari au ni wajibu?

Swali 2139: Je, kuziacha ndevu kukua na kupunguza masharubu ni Sunnah miongoni mwa Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ni miongoni mwa mambo yanayopendekezwa ambayo amehimiza?

Jibu: Kuacha ndevu za mwanaume zikue ni wajibu, kwa sababu ya amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu hilo. Kunyoa ndevu ni haramu, kwa sababu Mtume amekataza kunyoa na ameamuru kujitofautisha na washirikina katika jambo hilo. Msingi katika amri ni wajibu, na katika katazo ni uharamu.

Ama kupunguza masharubu au kuyapunguza sana ni miongoni mwa Sunnah za kimaumbile. Haijuzu kwa Muislamu kuyaacha yakiwa marefu, kwa sababu ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kutokata chochote katika masharubu yake si miongoni mwetu.”

Jengine ni kutokana na kwa ujumla wa Hadiyth zinazoamuru kuyapunguza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/140)
  • Imechapishwa: 23/10/2026