Mwanaume kumuoa mke wa baba wa mke wake

Swali: Je, inajuzu mwanamume kumuoa mke wa baba wa mke wake?

Jibu: Ndio, inajuzu mwanamume kumuoa mke wa baba wa mke wake ikiwa huyo si mama wa mke wake na hakuna uhusiano wa kunyonya kati yao. Hivyo anaweza kukusanya kati ya mwanamke na mke wa baba yake ambaye si mama yake. ´Abdullaah bin Ja´far alimuoa binti ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum) ambaye mama yake hakuwa huyo mke mwingine wa ´Aliy. Makusudio ni kwamba hakuna tatizo kukusanya wanawake wawili, mmoja akiwa ni mke wa baba wa mwingine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1359/حكم-الزواج-بزوجة-والد-الزوجة
  • Imechapishwa: 14/12/2025