Mwanamke uchiwazi kwenye TV – maafa ya zama hizi

Swali: Mwanamke wa Mashariki na wa Magharibi huonekana akiwa uchiwazi kwenye skrini ya TV mbele ya waislamu wanaume na wanawake. Nini unachosema juu ya fitina hii chafu?

Jibu: Hili ni miongoni mwa maafa yaliyotokana na TV; kuonekana kwa wanawake waliovaa lakini kimsingi wapo uchiwazi, pamoja na nyimbo nyingi na maigizo ya upotovu. Haya ni maafa na ni miongoni mwa sababu za kudorora kwa waislamu. Ni miongoni mwa mambo waliyowapenyezea maadui zao ili kuwafanya wadhoofike, kuwadhuru na kuharibu maadili yao. Hayo ni maovu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1456/ظهور-النساء-الكاسيات-العاريات-على-شاشات-التلفاز
  • Imechapishwa: 20/12/2025