Swali 1332: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa kile kinachoitwa wigi ili kujipamba kwa ajili ya mume wake?

Jibu: Inafaa kwa kila mmoja katika wanandoa kujipamba kwa ajili ya mwenzake kwa kile kinachomfanya akipende na kuimarisha mahusiano baina yao. Lakini iwe ndani ya mipaka ya yale ambayo Shari´ah ya Uislamu imeyaruhusu pasi na yale iliyoyaharamisha. Kuvaa kile kinachoitwa wigi kulianza miongoni mwa wanawake wasiokuwa waislamu na wakawa maarufu kwa kuivaa na kujipamba nayo mpaka ikawa miongoni mwa sifa zao. Kwa hiyo mwanamke kuivaa na kujipamba nayo, hata ikiwa ni kwa ajili ya mume wake, kuna kujifananisha na wanawake makafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo kwa kauli yake:

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu fulani, basi yeye ni miongoni mwao.”

Na pia wigi iko katika hukumu ya kuunga nywele, bali ni mbaya zaidi kuliko hiyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo na amemlaani mwenye kulifanya.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/191)
  • Imechapishwa: 27/10/2026