Swali: Je, kabla ya kutawadha mtu anatakiwa kutamka Basmalah au nia ya moyoni inatosha? Je, inapendekezwa kusoma Suurah “al-Qadr” baada ya kutawadha?
Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa mtu anapotaka kutawadha kuanza kwa kutamka Basmalah, huku nia ikiwa moyoni. Haitakiwi kuitamka nia kwa ulimi, kwa sababu kufanya hivyo ni miongoni mwa Bid´ah.
Ama kusoma Suurah “al-Qadr” baada ya kutawadha, hatujui dalili yoyote iliyothibiti kuhusu jambo hilo. Bali kilichowekwa katika Shari´ah baada ya kutawadha ni kusema:
أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمداً عبده ورسوله اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين
“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Ee Allaah! Nifanye kuwa miongoni mwa wenye kutubu na nifanye kuwa miongoni mwa wenye kujitwahirisha.”
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/203)
- Imechapishwa: 27/10/2026
Swali: Je, kabla ya kutawadha mtu anatakiwa kutamka Basmalah au nia ya moyoni inatosha? Je, inapendekezwa kusoma Suurah “al-Qadr” baada ya kutawadha?
Jibu: Ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa mtu anapotaka kutawadha kuanza kwa kutamka Basmalah, huku nia ikiwa moyoni. Haitakiwi kuitamka nia kwa ulimi, kwa sababu kufanya hivyo ni miongoni mwa Bid´ah.
Ama kusoma Suurah “al-Qadr” baada ya kutawadha, hatujui dalili yoyote iliyothibiti kuhusu jambo hilo. Bali kilichowekwa katika Shari´ah baada ya kutawadha ni kusema:
أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمداً عبده ورسوله اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين
“Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake. Ee Allaah! Nifanye kuwa miongoni mwa wenye kutubu na nifanye kuwa miongoni mwa wenye kujitwahirisha.”
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/203)
Imechapishwa: 27/10/2026
https://firqatunnajia.com/basmalah-kabla-ya-wudhuu-na-suurah-al-qadr-baada-yake/