Kukata nywele sehemu ya juu ya paji la uso na kufanya zingine zining’inie juu yake

Swali: Ni ipi hukumu ya mtindo wa nywele unaotumiwa na baadhi ya wanawake, ambao ni kukata nywele sehemu ya juu ya paji la uso na kufanya baadhi ya nywele zake zining’inie juu yake?

Jibu: Ikiwa lengo la mtindo huo wa nywele ni kujifananisha na wanawake makafiri na wenye wakanamungu, basi ni haramu. Kwa sababu kujifananisha na wasiokuwa waislamu ni haramu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote mwenye kujifananisha na watu fulani, basi yeye ni miongoni mwao.”

Ama ikiwa lengo si kujifananisha nao, bali ni desturi miongoni mwa desturi mpya zilizozoeleka baina ya wanawake, basi ikiwa ndani yake kuna jambo linalohesabiwa kuwa ni pambo ambalo anaweza kujipambia kwa ajili ya mume wake na kuonekana nalo mbele ya wanawake wenzake kwa mwonekano unaoongeza heshima yake mbele yao, basi hatuoni tatizo katika jambo hilo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/181)
  • Imechapishwa: 27/10/2026