Hakuna zakaah ndani yake mpaka anuie kufanya biashara nayo. Inapofikisha kile kiwango kinachowajibisha kutoa zakaah na ikazungukiwa na mwaka mmoja, hapo huikadiria thamani yake. Ikiwa imefikia kiwango cha chini cha kile kiwango cha zakaah cha dhahabu au fedha, basi atatoa zakaah kutokana na thamani yake. Ikiwa anayo dhahabu au fedha, basi ataijumuisha pamoja na thamani ya bidhaa za biashara katika kukamilisha kile kiwango cha zakaah. Ikiwa atanuia kutumia bidhaa za biashara kwa matumizi binafsi, basi hakuna zakaah ndani yake. Kisha ikiwa baadaye atanuia kufanya biashara nazo, huanza kuzihesabia mwaka mpya.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38
- Imechapishwa: 27/10/2026
Hakuna zakaah ndani yake mpaka anuie kufanya biashara nayo. Inapofikisha kile kiwango kinachowajibisha kutoa zakaah na ikazungukiwa na mwaka mmoja, hapo huikadiria thamani yake. Ikiwa imefikia kiwango cha chini cha kile kiwango cha zakaah cha dhahabu au fedha, basi atatoa zakaah kutokana na thamani yake. Ikiwa anayo dhahabu au fedha, basi ataijumuisha pamoja na thamani ya bidhaa za biashara katika kukamilisha kile kiwango cha zakaah. Ikiwa atanuia kutumia bidhaa za biashara kwa matumizi binafsi, basi hakuna zakaah ndani yake. Kisha ikiwa baadaye atanuia kufanya biashara nazo, huanza kuzihesabia mwaka mpya.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38
Imechapishwa: 27/10/2026
https://firqatunnajia.com/46-zakaah-ya-bidhaa-za-biashara/