Mwenye deni kwa mtu mwenye uwezo wa kulilipa, au mwenye mali ambayo anaweza kuipata – kama vile mtu anayekataa deni lake lakini mdai ana ushahidi wa kulithibitisha, au mali iliyonyakuliwa ambayo ana uwezo wa kuichukua – basi anawajibika kutoa zakaah yake anapoipokea, kwa miaka iliyopita. Ama ikiwa ni mali ambayo kuipata ni kugumu, kama deni alilopewa mtu aliyefilisika, mtu anayekataa deni hilo bila kuwa na ushahidi wa kulithibitisha, mali iliyonyakuliwa au mali iliyopotea ambayo hakuna matumaini ya kuipata, basi hakuna zakaah ndani yake.’

Mahari yana hukumu moja kama deni.

Mwenye deni ambalo rasilimali yake inalingana au linapunguza kile kiwango cha zakaah, basi hatotoa zakaah.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 37
  • Imechapishwa: 27/10/2026