Nayo ni aina mbili: dhahabu na fedha.

Hakuna zakaah katika fedha mpaka zifikie thamani ya dirhamu 200. Zikifikia thamani ya dirhamu 200, basi inawajibika kutoa dirhamu 5.

Hakuna zakaah katika dhahabu mpaka ifikie thamani ya gramu 82. Ikifikia thamani ya gramu 82, basi inawajibika kutoa gramu 2,5.

Ikiwa dhahabu au fedha imechanganywa na kitu kingine, hakuna zakaah ndani yake mpaka kiasi cha dhahabu au fedha kifikie kile kiwango cha zakaah. Ikiwa mtu ana shaka kuhusu kiasi hicho, basi ana uchaguzi wa kutoa zakaah au kuviyeyusha ili ajue kiasi cha dhahabu au fedha kilichomo.

Hakuna zakaah katika mapambo yanayoruhusiwa ambayo yametayarishwa kwa ajili ya matumizi na kukopeshwa.

Wanawake wanaruhusiwa kuvaa kila aina ya mapambo ya dhahabu na fedha ambayo kwa desturi huvaliwa. Wanaume wanaruhusiwa katika fedha kuvaa pete, mapambo ya upanga, mkanda wa kiunoni na mfano wa hayo. Ama mapambo yaliyotayarishwa kwa ajili ya kukodishwa au kuhifadhiwa na mapambo yaliyoharamishwa, basi yanatolewa zakaah.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 37
  • Imechapishwa: 27/10/2026