Mwanamke kupunguza mavazi yake anapokuwa na wanawake wenzake

Swali: Dada muislamu anavaa nguo inayofunika mwili wote na isiyo nyepesi, kisha anavaa ´Abaa´ah ambayo pia inafunika nguo yote mpaka ardhini, imefungwa mbele na pia anafunika uso wake. Je, inajuzu kwake kuvua ´Abaa´ah pekee anapowatembelea baadhi ya wanawake waislamu? Ni ipi hukumu na na ni ipi dalili?

Jibu: Hakika mwanamke ni uchi na hivyo ni lazima ajisitiri mbele ya wanaume wasiokuwa Mahram. Ama akiwatembelea wanawake, hapana vibaya. Kwa sababu si lazima ajisitiri mbele ya wanawake. Bali atajisitiri mbele ya wanaume. Hivyo basi akiwatembelea wanawake na akaondoa ´Abaa´ah yake, hapana vibaya wala shida yoyote kufanya hivo. Allaah amesema:

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

”Mnapowauliza haja, basi waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.”[1]

وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ

“Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, baba zao, baba za waume wao, wana wao wa kiume, wana wa kiume wa waume zao, kaka zao, wana wa kiume wa kaka zao, wana wa kiume wa dada zao, wanawake wao [dada zao wa Kiislamu]… “[2]

Kwa hiyo kuonesha mapambo kwa wanawake hapana tatizo wala neno kufanya hivo.

[1] 33:53

[2] 24:31

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30114/حكم-خلع-المراة-حجابها-عند-النساء
  • Imechapishwa: 11/09/2025