Swali: Kuna mwanamke ameolewa miaka saba iliyopita na ripoti za kidaktari zimethibitisha kuwa mume wake hana uzazi. Je, anaweza kumuomba talaka mume wake huyu ambaye hana uzazi? Unamnasihi nini?
Jibu: Ndio, inafaa kwake kuomba talaka. Kwa sababu ana haki ya kupata watoto. Ikithibiti kuwa kweli mume wake ni tasa, basi ana haki ya kufuta talaka. Lakini kunabaki kitu kimoja; je, lililo bora ni yeye kuomba kufutwa kwa ndoa au bora ni yeye kubaki pamoja naye? Anatakiwa kutazama. Ikiwa mwanamume huyu ni mtu wa kheri, wa dini na wa tabia, basi ni sawa akabaki pamoja naye. Vinginevyo lililo bora ni yeye kutafuta mume ambaye anaweza kupata naye watoto. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Oeni wanawake wenye kuzaa sana na wenye mahaba.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/827
- Imechapishwa: 14/03/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Mwanamke aombe talaka kwa mume ambaye ni tasa?
Swali: Wanandoa wengi wanaishi pasi na watoto na hilo ni kwa sababu ya tatizo liliopo kwa mume. Je, bora ni mume kutafuta matibabu pamoja na kusubiri na kuatarajia malipo kutoka kwa Allaah au atafute mwanamke mwingine badala? Jibu: Hapana shaka kwamba kuchelewa kupata mtoto kunawezekana ni kwa sababu mwanaume huyo…
In "Khul´ (Mwanamke kujivua katika ndoa)"

Mke kuomba talaka kwa mume wake bila ya sababu yoyote
https://www.youtube.com/watch?v=5GIHzJs8Bio Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuomba Talaka kwa mume wake na lini anaweza kuomba? Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Mwanamke yeyoye atakayeomba Talaka kutoka kwa mume wake bila ya sababu yoyote, ni kaharamishiwa harufu ya Pepo." Tunachomnasihi ni yeye kuwa na subira, na subira…
In "Khul´ (Mwanamke kujivua katika ndoa)"
Mke anataka kubaki nyumbani kwao baada ya ndoa
Swali: Wakati mtu anapooa na kukamilisha zile sharti zinazomlazimu kisha mwanaume anataka kumchukua mke wake mlezi wa mwanamke huyu anamkatalia. Vinginevyo anamuhudumia na harusiwi kwenda nyumbani kwake. Mwanaume anakuwa na kazi ya kwenda na kurudi nyumbani kwa baba yake mdogo ambaye ndiye mlezi wa msichana huyu. Mume akimwacha mke wake…
In "Matangamano na maelewano kati ya mume na mke"