Swali: Ni ipi hekima ya mwanamke kufunua uso wake na mikono yake wakati wa kutekeleza ´ibaadah za Hajj?
Jibu: Hana ruhusa ya kufanya hivyo. Bali ni wajibu kwake kufunika uso wake na mikono yake hata katika Hajj. Isipokuwa hatakiwi kuvaa Niqaab inayojulikana, bali afunike uso wake kwa kitu kingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza kuvaa Niqaab, lakini hakumkataza mwanamke kufunika uso wake. Bali alimkataza Niqaab na vifuniko vya mikono katika hali ya Ihraam. Maana yake ni kwamba afunike uso wake kwa kitu kingine kama Khimaar au Jilbaab. Hivyo ndivo ilivyosimuliwa kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
”Walikuwa wanafikiwa na wanaume, basi mmoja wao hushusha Khimaar yake juu ya uso wake na wakiondoka hufunua.”
Vivyo hivyo inapokuja katika mikono ambayo hatakiwi kuvaa vifuniko vya mikono. Lakini anaweza kufunika mikono yake kwa Jilbaab, ´Abaa´ah au Khimaar. Ni ilivyo kwa mwanaume ambaye haifai kwake kuvaa kanzu wala hafuniki kichwa chake ndani ya Ihraam. Lakini anafunika mwili wake kwa shuka ya chini na anafunika mwili wake kwa shuka ya juu na pia anaweza kufunika mikono yake kwa shuka ya juu, jambo ambalo halina ubaya. Mwanamke pia anavaa kanzu yake ya kike na anafunika kichwa chake. Lakini hafuniki uso wake kwa Niqaab na wala hafuniki mikono yake kwa vifuniko vya mikono. Bali anafunika uso wake kwa Jilbaab au kwa Khimaar wakati wanapokuwepo wanaume. Aidha anafunika mikono yake kwa Khimaar yake, kwa ´Abaa´ah yake au kwa Jilbaab yake. Hii ndiyo tofauti kati ya mambo mawili.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3175/حكم-كشف-المراة-وجهها-وكفيها-اثناء-الحج
- Imechapishwa: 25/10/2026
Swali: Ni ipi hekima ya mwanamke kufunua uso wake na mikono yake wakati wa kutekeleza ´ibaadah za Hajj?
Jibu: Hana ruhusa ya kufanya hivyo. Bali ni wajibu kwake kufunika uso wake na mikono yake hata katika Hajj. Isipokuwa hatakiwi kuvaa Niqaab inayojulikana, bali afunike uso wake kwa kitu kingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataza kuvaa Niqaab, lakini hakumkataza mwanamke kufunika uso wake. Bali alimkataza Niqaab na vifuniko vya mikono katika hali ya Ihraam. Maana yake ni kwamba afunike uso wake kwa kitu kingine kama Khimaar au Jilbaab. Hivyo ndivo ilivyosimuliwa kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
”Walikuwa wanafikiwa na wanaume, basi mmoja wao hushusha Khimaar yake juu ya uso wake na wakiondoka hufunua.”
Vivyo hivyo inapokuja katika mikono ambayo hatakiwi kuvaa vifuniko vya mikono. Lakini anaweza kufunika mikono yake kwa Jilbaab, ´Abaa´ah au Khimaar. Ni ilivyo kwa mwanaume ambaye haifai kwake kuvaa kanzu wala hafuniki kichwa chake ndani ya Ihraam. Lakini anafunika mwili wake kwa shuka ya chini na anafunika mwili wake kwa shuka ya juu na pia anaweza kufunika mikono yake kwa shuka ya juu, jambo ambalo halina ubaya. Mwanamke pia anavaa kanzu yake ya kike na anafunika kichwa chake. Lakini hafuniki uso wake kwa Niqaab na wala hafuniki mikono yake kwa vifuniko vya mikono. Bali anafunika uso wake kwa Jilbaab au kwa Khimaar wakati wanapokuwepo wanaume. Aidha anafunika mikono yake kwa Khimaar yake, kwa ´Abaa´ah yake au kwa Jilbaab yake. Hii ndiyo tofauti kati ya mambo mawili.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3175/حكم-كشف-المراة-وجهها-وكفيها-اثناء-الحج
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/mwanamke-kufunua-uso-wake-wakati-wa-kutekeleza-ibaadah-za-hajj-au-umrah/