Swali: Imekuja katika maneno ya Shaykh wa al-Azhar katika moja ya magazeti ya Misri kwamba uso si uchi kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi wa Kiislamu. Je, hili ni sahihi kwamba maoni ya wengi wa wanazuoni yanaruhusu kufunua uso? Na pia, ikiwa mwenye mamlaka katika uwanja wa ndege atamtaka mwanamke kufunua uso wake kwa hoja ya kuthibitisha utambulisho wake, je, anapaswa kutii katika hilo?
Jibu: Maoni ya kusema kuwa hii ni maoni ya wanazuoni wengi yanahitaji kuangaliwa kwa makini na kuchunguzwa. Mara nyingi hudaiwa kuwa jambo fulani ni maoni ya wengi ilihali si hivyo. Si Shaykh wa al-Azhar peke yake aliyesema hili, bali wamesema pia watu wengine katika wanazuoni. Lakini wamekosea katika hilo. Haifai kwa mwenye akili kudanganyika na maoni ya fulani au fulani, bali masuala ya makinzano yanapaswa kurejeshwa katika yale aliyosema Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na dalili za Kishari´ah. Dalili zimeonyesha ulazima wa Hijaab, wajibu wa mwanamke kujifunika mwili wake na kujiepusha na sababu za fitina, kwani hilo ni usafi zaidi kwa nyoyo za wanaume na wanawake. Hivyo yale yaliyopokelewa kutoka kwa Shaykh wa al-Azhar na wengine pamoja na yaliyoandikwa na ´Allaamah Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy katika kitabu chake “al-Hijaab” na yaliyoandikwa na wengine, yote hayo yanapaswa kupimwa kwa Qur-aan na Sunnah. Tulipoyapima kwa Qur-aan na Sunnah tukakuta kuwa aliyesema kufunua Hijaab amekosea na aliyesema Hijaab ni wajibu amepatia. Ikiwa aliyesema kufunua Hijaab na kuruhusu mwanamke kufunua uso alimtakasia nia Allaah na alikusudia haki, lakini akakosea kwa ijtihadi yake bila ya kufuata matamanio wala kupuuza, basi atapata thawabu ya ijtihadi na Allaah atamsamehe, lakini atakosa kupata ujira wa kupatia. Ama aliyefuata matamanio na shari, basi hatapata hili wala lile, bali atapata dhambi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3173/الرد-على-ادعاء-ان-كشف-المراة-وجهها-هو-قول-الجمهور
- Imechapishwa: 25/10/2026
Swali: Imekuja katika maneno ya Shaykh wa al-Azhar katika moja ya magazeti ya Misri kwamba uso si uchi kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi wa Kiislamu. Je, hili ni sahihi kwamba maoni ya wengi wa wanazuoni yanaruhusu kufunua uso? Na pia, ikiwa mwenye mamlaka katika uwanja wa ndege atamtaka mwanamke kufunua uso wake kwa hoja ya kuthibitisha utambulisho wake, je, anapaswa kutii katika hilo?
Jibu: Maoni ya kusema kuwa hii ni maoni ya wanazuoni wengi yanahitaji kuangaliwa kwa makini na kuchunguzwa. Mara nyingi hudaiwa kuwa jambo fulani ni maoni ya wengi ilihali si hivyo. Si Shaykh wa al-Azhar peke yake aliyesema hili, bali wamesema pia watu wengine katika wanazuoni. Lakini wamekosea katika hilo. Haifai kwa mwenye akili kudanganyika na maoni ya fulani au fulani, bali masuala ya makinzano yanapaswa kurejeshwa katika yale aliyosema Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na dalili za Kishari´ah. Dalili zimeonyesha ulazima wa Hijaab, wajibu wa mwanamke kujifunika mwili wake na kujiepusha na sababu za fitina, kwani hilo ni usafi zaidi kwa nyoyo za wanaume na wanawake. Hivyo yale yaliyopokelewa kutoka kwa Shaykh wa al-Azhar na wengine pamoja na yaliyoandikwa na ´Allaamah Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy katika kitabu chake “al-Hijaab” na yaliyoandikwa na wengine, yote hayo yanapaswa kupimwa kwa Qur-aan na Sunnah. Tulipoyapima kwa Qur-aan na Sunnah tukakuta kuwa aliyesema kufunua Hijaab amekosea na aliyesema Hijaab ni wajibu amepatia. Ikiwa aliyesema kufunua Hijaab na kuruhusu mwanamke kufunua uso alimtakasia nia Allaah na alikusudia haki, lakini akakosea kwa ijtihadi yake bila ya kufuata matamanio wala kupuuza, basi atapata thawabu ya ijtihadi na Allaah atamsamehe, lakini atakosa kupata ujira wa kupatia. Ama aliyefuata matamanio na shari, basi hatapata hili wala lile, bali atapata dhambi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3173/الرد-على-ادعاء-ان-كشف-المراة-وجهها-هو-قول-الجمهور
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/maoni-yanayosema-kuwa-kufunika-uso-si-lazima/