Swali: Kuhusu watoto ambao hawajafikia umri wa kupambanua mambo, je, inafaa wasimame katika safu ya kwanza nyuma ya imamu, mfano mwenye miaka mitano au sita?
Jibu: Kinachodhihiri ni kwamba hawapaswi kuwekwa pamoja na safu za wanaoswali, kwa sababu bado si katika watu wa swalah. Watu wa swalah ni wale wenye miaka isiyopungua saba, kama ilivyokuja katika Hadiyth:
“Waamrisheni watoto wenu swalah wakiwa na miaka saba na wapigeni kwayo wanapofikia miaka kumi.”
Ama aliye chini ya miaka saba, basi si katika watu wa swalah. Isitoshe huenda akawashawishi wanaoswali au kuwaudhi. Hivyo haifai awe pamoja na wanaoswali, bali ni bora abakie nyumbani.
Swali: Wakati mwingine tunawaweka watoto wa kiume kati ya wanaume ili wasichanganyike wao kwa wao na kucheza katika swalah?
Jibu: Hii ni katika njia ya kutatua tatizo. Ikiwa kuna khofu ya kucheza au kufanya vurugu, basi awekewe mtu mzima kati yao; kila watoto wawili wawe na mtu mzima kati yao ili wasicheze.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3191/حكم-وقوف-الاطفال-دون-سن-السابعة-في-الصف
- Imechapishwa: 25/10/2026
Swali: Kuhusu watoto ambao hawajafikia umri wa kupambanua mambo, je, inafaa wasimame katika safu ya kwanza nyuma ya imamu, mfano mwenye miaka mitano au sita?
Jibu: Kinachodhihiri ni kwamba hawapaswi kuwekwa pamoja na safu za wanaoswali, kwa sababu bado si katika watu wa swalah. Watu wa swalah ni wale wenye miaka isiyopungua saba, kama ilivyokuja katika Hadiyth:
“Waamrisheni watoto wenu swalah wakiwa na miaka saba na wapigeni kwayo wanapofikia miaka kumi.”
Ama aliye chini ya miaka saba, basi si katika watu wa swalah. Isitoshe huenda akawashawishi wanaoswali au kuwaudhi. Hivyo haifai awe pamoja na wanaoswali, bali ni bora abakie nyumbani.
Swali: Wakati mwingine tunawaweka watoto wa kiume kati ya wanaume ili wasichanganyike wao kwa wao na kucheza katika swalah?
Jibu: Hii ni katika njia ya kutatua tatizo. Ikiwa kuna khofu ya kucheza au kufanya vurugu, basi awekewe mtu mzima kati yao; kila watoto wawili wawe na mtu mzima kati yao ili wasicheze.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3191/حكم-وقوف-الاطفال-دون-سن-السابعة-في-الصف
Imechapishwa: 25/10/2026
https://firqatunnajia.com/mtoto-chini-ya-miaka-saba-katika-safu/