Swali: Inajuzu kwangu kufunua uso wangu mbele ya ndugu wa mume wangu ilihali najua kuwa ni haramu pamoja na kuwa kuna uzito mkubwa unaonizuia kufanya hivo? Mimi hujisitiri isipokuwa uso wangu ambao hubaki wazi pamoja na kujua kwamba mimi sikai nao isipokuwa tu wakati wa chakula.

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kufunua uso wake mbele ya ndugu zake mume wala mbele ya wajomba wa mumewe. Hawa sio Mahaarim zake. Ni lazima kwake kuwa na subira hata kama watamuudhi. Anatakiwa afanye subira. Kile kitendo chake kwamba hafuniki uso wake na wakati huohuo anafunika sehemu iliyobaki ya mwili ni kosa analofanya. Kwa sababu uso una haki zaidi kuliko viungo vyengine vya mwili mbele ya ambao sio Mahaarim kwa usoni ndio sehemu ya uzuri kwa mwanamke na ndipo kunakuwa fitina. Wanamme wanapotaka kumchumbia mwanamke hutazama nini; uso au miguu? Hutazama usoni. Hutompata mwanaume yeyote wakati anapotaka kuchumbia anasema – na kwa hali yoyote hatomuwakilisha yeyote isipokuwa mmoja katika Mahaarim zake yule mwanamke kama mfano wa kaka yake ambaye huenda akawa ni rafiki yake: –  Ndugu! Nieleze kuhusu miguu ya dada yako au huuliza uso? Pasi na shaka huuliza uso. Masuala haya hata kama wasingekuwepo wanachuoni wakubwa wenye kuonelea hivo, basi akili ilikuwa ni yenye kupelekea kwamba ni haramu kwa mwanamke kutoka hali ya kuwa amefunua miguu yake, basi kuharamika kuonekana kwa uso kungeliwa ni aula zaidi. Hili halina shaka. Lau tungelitumia akili tu basi mtu angeliweza kusema kwamba haiwezekani mwanamke kuacha uso wake wazi ikawa ni halali na nyayo zake ikawa haramu. Pamoja na kuwa Shari´ah inapelekea juu ya uwajibu wa mwanamke kufunika uso wake mbele ya ambao si Maharam zake.

Namwambia mwanamke huyu: Allaah akujaze. Namwambia awe na subira na atarajie malipo kutoka kwa Allaah na akumbuke maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ

”Miongoni mwa watu wako wasemao “Tumemwamini Allaah”; lakini wanapofanyiwa maudhi kwa ajili ya Allaah, hufanya mitihani ya watu kama kwamba ni adhabu ya Allaah.”[1]

Asubiri na achunge ahadi ya Allaah (´Azza wa Jall):

فَاصْبِرْ ۖ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ

“Basi subiri, hakika mwisho mwema ni kwa wenye kumcha Allaah.”[2]

[1] 29:10

[2] 11:49

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1590
  • Imechapishwa: 29/05/2020