Mwanamke amepita mbele ya imamu ambaye hakuwa na Sutrah

Swali: Tuliswali Maghrib na imamu hakuwa na Sutrah, kisha akapita mwanamke mbele yake kwa umbali wa takriban mita mbili. Ni ipi hukumu? Je, swalah yetu ni sahihi au si sahihi?

Jibu: Ikiwa kulikuwa kati yake na huyo mwanamke takriban dhiraa tatu, basi haidhuru. Lakini ikiwa ni chini ya hapo, basi kunaharibu swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali kuelekea ukuta wa Ka´bah na kati yake na ukuta kulikuwa na dhiraa tatu. Kundi la wanazuoni wamejengea dalili kutokana na hilo kwamba dhiraa tatu ndiyo mpaka wa mwisho ikiwa mtu hana Sutrah. Ama ikiwa mtu anayo Sutrah, basi swalah yake haiharibiki isipokuwa kama mtu atapita kati yake na Sutrah. Ikiwa mwanamke alipita mbele yake bila kuwepo Sutrah – na umbali ulikuwa mita mbili, ambayo ni zaidi ya dhiraa tatu – basi huenda swalah haiharibiki – Allaah akitaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/126)
  • Imechapishwa: 04/03/2026