Mwanamke aliyesimuli anapokuwa hana walii muislamu

Swali: Vipi ikiwa mwanamke amesilimu na yuko na walii kafiri?

Jibu: Kafiri hana usimamizi. Lakini ikiwa mwanamke hana budi na wakati huohuo hana walii, ni sawa akamsimamia kama walii ili kusitokee mtihani. Atamsimamia kama walii. Ukweli wa mambo ni kwamba mwanamke huyu atakuwa amejiozesha mwenyewe. Hata hivyo kutokana na dharurah amshauri ili kusitokee kati yake na mume wake fitina na ili kusitokee shari. Vinginevyo sio walii anayezingatiwa kwa mujibu wa Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23833/حكم-تزويج-من-كان-وليها-كافرا
  • Imechapishwa: 08/05/2024