Swali: Mwalimu wa kike alituusia jambo la amana kwenye shingo zetu ambayo tutaulizwa juu yake siku ya Qiyaamah, nalo ni kwamba tusimpe mwanafunzi mwengine juhudi zetu binafsi ili kila mmoja ajifunze mwenyewe kutatua tatizo. Siku ya pili baadhi ya wenzangu walikuja kwangu wakitaka niwaandikie kuhusu utambulisho wa Uislamu katika somo la lugha ya kingereza. Hiyo ndiyo amana ambayo mwalimu alituamrisha. Lakini kwa hakika shaytwaan – Allaah amlaani – alinisahaulisha amana hiyo na nikaanza kuwaandikia. Je, nina dhambi kwa kufanya hivyo, hali ya kuwa nilikuwa nimesahau? Kama nitamwambia mwalimu hatanisamehe. Je, ana haki ya kufanya hivyo?
Jibu: Ushirikiano baina ya wanafunzi ni jambo sahihi. Ushirikiano katika kunufaishana, kutafiti na kujadiliana. Ama jambo la siri, kama maswali ambayo mmeambiwa msiyatoe majibu yake ili kila mwanafunzi ajitahidi, basi usimwambie. Mwache ajitahidi, atafute na kuuliza kwa bidii. Lakini tafiti za jumla baina yao katika masuala ya elimu na kupata manufaa, hilo ni jambo sahihi. Lakini maswali ya siri ambayo mnajua kuwa ni siri, si haki ya mmoja kumwambia mwingine, kwa sababu ikiwa atamwambia na akapuuza, basi mwanafunzi hatakuwa na juhudi, hatatafuta wala hatajitahidi. Matokeo yake atakuwa mfuasi wa mwingine. Kwa hiyo ni wajibu kumwacha ajitahidi na kutafuta. Ama tafiti za jumla baina ya wanafunzi, basi kila mmoja ajitahidi kumfahamisha mwenzake jambo ambalo anaweza kuwa halijui, ajitahidi kumnasihi, kumwelekeza na kumfundisha namna ya kufanya utafiti sahihi katika kitabu hiki na kile na mfano wa hayo ya kushirikiana. Lakini jambo la siri ambalo mnajua kuwa ni siri na walimu wamekwishakwambia kuwa ni siri, basi usimwambie. Kila mmoja ajitahidi.
Swali: Je, kuna dhambi ninayopata?
Ibn Baaz: Haidhuru muda wa kuwa ulikuwa umesahau:
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]
[1] 02:286
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30918/ما-الذي-يجوز-للطلبة-التعاون-فيه-في-الدراسة
- Imechapishwa: 15/09/2025
Swali: Mwalimu wa kike alituusia jambo la amana kwenye shingo zetu ambayo tutaulizwa juu yake siku ya Qiyaamah, nalo ni kwamba tusimpe mwanafunzi mwengine juhudi zetu binafsi ili kila mmoja ajifunze mwenyewe kutatua tatizo. Siku ya pili baadhi ya wenzangu walikuja kwangu wakitaka niwaandikie kuhusu utambulisho wa Uislamu katika somo la lugha ya kingereza. Hiyo ndiyo amana ambayo mwalimu alituamrisha. Lakini kwa hakika shaytwaan – Allaah amlaani – alinisahaulisha amana hiyo na nikaanza kuwaandikia. Je, nina dhambi kwa kufanya hivyo, hali ya kuwa nilikuwa nimesahau? Kama nitamwambia mwalimu hatanisamehe. Je, ana haki ya kufanya hivyo?
Jibu: Ushirikiano baina ya wanafunzi ni jambo sahihi. Ushirikiano katika kunufaishana, kutafiti na kujadiliana. Ama jambo la siri, kama maswali ambayo mmeambiwa msiyatoe majibu yake ili kila mwanafunzi ajitahidi, basi usimwambie. Mwache ajitahidi, atafute na kuuliza kwa bidii. Lakini tafiti za jumla baina yao katika masuala ya elimu na kupata manufaa, hilo ni jambo sahihi. Lakini maswali ya siri ambayo mnajua kuwa ni siri, si haki ya mmoja kumwambia mwingine, kwa sababu ikiwa atamwambia na akapuuza, basi mwanafunzi hatakuwa na juhudi, hatatafuta wala hatajitahidi. Matokeo yake atakuwa mfuasi wa mwingine. Kwa hiyo ni wajibu kumwacha ajitahidi na kutafuta. Ama tafiti za jumla baina ya wanafunzi, basi kila mmoja ajitahidi kumfahamisha mwenzake jambo ambalo anaweza kuwa halijui, ajitahidi kumnasihi, kumwelekeza na kumfundisha namna ya kufanya utafiti sahihi katika kitabu hiki na kile na mfano wa hayo ya kushirikiana. Lakini jambo la siri ambalo mnajua kuwa ni siri na walimu wamekwishakwambia kuwa ni siri, basi usimwambie. Kila mmoja ajitahidi.
Swali: Je, kuna dhambi ninayopata?
Ibn Baaz: Haidhuru muda wa kuwa ulikuwa umesahau:
رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]
[1] 02:286
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30918/ما-الذي-يجوز-للطلبة-التعاون-فيه-في-الدراسة
Imechapishwa: 15/09/2025
https://firqatunnajia.com/mwanafunzi-ameenda-kinyume-na-amri-ya-mwalimu-kumwambia-mwenzake-asiyotakiwa-kuyasema/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket