Muuguzi kumfanyisha Tayammum mgonjwa

Swali: Vipi mzima kumfanyisha Tayammum ambaye ni mgonjwa?

Jibu: Ni lazima atie nia. Ni lazima mgonjwa anuie kama ambavo anamtawadhisha kwa maji. Mgonjwa anuie Tayammum na muuguzi ampanguse uso na mikono yake kwa udongo.

Swali: Baadhi yao wanamfanyisha Tayammum mgonjwa pasi na kuwaambia?

Jibu: Haisihi. Ni lazima atie nia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24135وجوب-النية-اذا-يمم-الصحيح-المريض
  • Imechapishwa: 06/09/2024