Mume usifanye uzazi wa mpango bila ya idhini ya mke

Swali: Je, ni lazima kwa mume kumuomba idhini mke wakati wa kuchomoa kabla ya kumwaga?

Jibu: Maoni ya karibu zaidi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba ni lazima kufanya hivo. Kwa sababu mwanamke anayo haki ya kupata watoto. Kumepokelewa Hadiyth ambayo ni dhaifu inayosema amtake ruhusa. Lakini maana yake iko wazi. Haifai kwake kuchomoa kabla ya kumwaga isipokuwa kwa idhini yake. Isipokuwa akiwa ni mjakazi hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23892/هل-يلزم-الزوج-استىذان-الزوجة-عند-العزل
  • Imechapishwa: 27/05/2024