Mume hulazimiki kumtaliki mke wako anayedai talaka unapoongeza mke mwengine

Swali: Ikiwa mke wa kwanza amekataa kuishi na wa pili baada ya ndoa na akaomba talaka. Ni ipi hukumu ya talaka?

Jibu: Sio lazima kwake mume kumtaliki. Ni lazima kwa mwanamke huyo kunyenyekea hukumu ya Allaah na asubiri.

Swali: Ameomba talaka na amekataa kurudi?

Jibu: Hapana vibaya akitaka kumtaliki. Hata hivyo mume halazimiki kufanya hivo. Hapana vibaya kama anataka kumtaliki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23898/هل-تطلق-الزوجة-لرفضها-العيش-مع-اخرى
  • Imechapishwa: 29/05/2024