Swali: Ni ipi hukumu ya mtu aliye katika Ihraam kuweka juu ya kichwa chake mwavuli uliowekwa imara unaozunguka pamoja na kichwa ukiwa umetundikwa juu ya kichwa?

Jibu: Ikiwa umeunganishwa na mwili na umefungwa juu yake, basi haijuzu. Ama ikiwa anaushika kwa mkono wake, basi hakuna tatizo kujisitiri kwa kivuli chake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 27/09/2026