Muhimu yawe manyonyesho matano

Swali: Nini maana ya manyonyesha matano yenye kushibisha?

Jibu: Manyonyesha hata kama si yenye kushibisha. Hakuna yeyote anayesema lazima yashibishe. Muhimu yawe manyonyesha matano hata kama hayashibishi. Ikiwa mtoto mchanga atanyonya na akameza maziwa na maziwa yakafika tumboni mwake [mtoto amekuwa mwanae], hata kama hakushiba. Hiyo inahesabiwa kuwa ni kunyonya mara moja. Kisha akarudia na kunyonya kwa mara ya pili, hata kama hakushiba, inahesabiwa kuwa ni kunyonya mara ya pili na kadhalika. Si sharti manyonyesho yawe yenye kushibisha.

Swali: Hata ndani ya kikao kimoja?

Ibn Baaz: Hata ndani ya kikao kimoja au katika vikao vingi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29380/ما-معنى-خمس-رضعات-مشبعات
  • Imechapishwa: 02/08/2025