Muhammad bin Ibraahiym kuhusu kusherehekea krismasi na mwaka mpya

Tumefikiwa na khabari kwamba baadhi ya wafanyabiashara waliingiza nchini zawadi maalum kwa mnasaba wa sikukuu ya krismasi. Miongoni kwa zawadi hizi kulikuweko mti wa kuzaliwa kwa al-Masiyh na kwamba baadhi ya wananchi walikuwa wakiinunua na wakiwapa wageni wa kikristo nchini mwetu kwa ajili ya kushirikiana kwao katika sikukuu hii. Kitendo hichi ni cha dhambi na haikutakiwa kwao kukifanya. Hatuna shaka kwamba nyinyi pia mnajua kuwa jambo hilo halijuzu na yale yaliyotajwa na wanachuoni walipokubaliana juu ya ukhatari wa kushirikina na makafiri katika washirikina na Ahl-ul-Kitaab katika sikukuu zao. Tunataraji mtazingatia kuzuia yale yanayoingizwa nchini katika zawadi hizi na vyenginevyo vilivyo katika hukumu yake miongoni mwa vitu ambavyo ni maalum katika sikukuu zoa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (3/105) http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=2988
  • Imechapishwa: 18/12/2019