Swali: Mara nyingi nasafiri kwa treni kwa umbali mrefu. Katika safari hiyo hupita wakati wa swalah mbili au tatu. Kwa sababu ya ufinyu wa nafasi ndani ya treni sipati mahali pa kuswali. Je, nizikusanye swalah hizi kwa kuzikusanya mwanzo wa wakati au kwa kuzikusanya mwisho wa wakati au niswali kila swalah nikiwa nimekaa katika kiti changu?
Jibu: Ni wajibu kwako na kwa abiria wote wa treni miongoni mwa waislamu kuswali swalah ndani ya wakati wake. Pia wanaruhusiwa kukusanya swalah ya Dhuhr pamoja na ´Aswr, Maghrib pamoja na ´Ishaa katika wakati wa mojawapo yao ikiwa wako safarini. Wanapaswa kuswali kadiri ya uwezo wao; wakiwa wamesimama au wakiwa wamekaa. Ikiwa hawawezi kurukuu au kusujudu, basi wataashiria kwa ishara ambapo wafanye sujuud iwe chini zaidi kuliko Rukuu´. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Pia ni wajibu kwa dereva wa treni kuwafanyia wepesi na kusimama nao katika sehemu zinazofaa ili waweze kuswali swalah ndani ya wakati wake.
[1] 64:16
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/192)
- Imechapishwa: 10/03/2026
Swali: Mara nyingi nasafiri kwa treni kwa umbali mrefu. Katika safari hiyo hupita wakati wa swalah mbili au tatu. Kwa sababu ya ufinyu wa nafasi ndani ya treni sipati mahali pa kuswali. Je, nizikusanye swalah hizi kwa kuzikusanya mwanzo wa wakati au kwa kuzikusanya mwisho wa wakati au niswali kila swalah nikiwa nimekaa katika kiti changu?
Jibu: Ni wajibu kwako na kwa abiria wote wa treni miongoni mwa waislamu kuswali swalah ndani ya wakati wake. Pia wanaruhusiwa kukusanya swalah ya Dhuhr pamoja na ´Aswr, Maghrib pamoja na ´Ishaa katika wakati wa mojawapo yao ikiwa wako safarini. Wanapaswa kuswali kadiri ya uwezo wao; wakiwa wamesimama au wakiwa wamekaa. Ikiwa hawawezi kurukuu au kusujudu, basi wataashiria kwa ishara ambapo wafanye sujuud iwe chini zaidi kuliko Rukuu´. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Pia ni wajibu kwa dereva wa treni kuwafanyia wepesi na kusimama nao katika sehemu zinazofaa ili waweze kuswali swalah ndani ya wakati wake.
[1] 64:16
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/192)
Imechapishwa: 10/03/2026
https://firqatunnajia.com/muda-wa-swalah-unampita-kwa-kisingizio-cha-safari-ndefu/