Muadhini anasoma du´aa ya baada ya adhaana kwa sauti ya juu

Swali: Baada ya muadhini kuadhini anasoma ile du´aa iliyopokelewa baada ya adhaana kwenye kipasa sauti. Je, kuna kosa katika kufanya hivo?

Jibu: Ndio, ni kosa. Muadhini akisoma ile du´aa iliyosuniwa kwenye kipaza sauti inaleta hisia fulani kana kwamba ni sehemu katika adhaana. Jengine ni kwamba jambo hilo halikuwa lenye kutambulika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makhaliyfah wake waongofu. Kwa hiyo ni katika Bid´ah zilizokemewa. Hata kama mtu atasema kuwa malengo yake ni kuwafunza watu, tunamwambia kuwa anaweza kuwafunza watu du´aa hii baada ya adhaana hata kama ni kwa njia ya kipaza sauti. Waeleze kuwa mtu anatakiwa kusema kadhaa na kadhaa baada ya kumalizika adhaana. Asiseme kwa sauti ya juu baada ya adhaana, kwa njia ya kwamba watu wakaanza kufikiria kuwa ni sehemu katika adhaana. Kitendo hicho ni katika Bid´ah.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/198)
  • Imechapishwa: 05/04/2026