Swali: Je, kijakazi anaruhusiwa kwa bwana wake kumjamii, basi je, mtumwa mwanaume anaruhusiwa kumjamii bibi yake kwa idhini yake kutokana na maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ
”… isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.”[1]
Jibu: Hapana, jambo hili ni maovu. Hili lililokuja katika Aayah linahusu wanaume, kama alivyosema (Ta´ala):
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
“Na ambao wanazihifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume basi hao hawalaumiwi.” (23:05-06)
Makusudio yake ni wajakazi kwa bwana wao. Ndiyo maana wametajwa pamoja na wake zao halali. Hivyo basi bwana anaruhusiwa kumuingilia mke wake wa ndoa na pia kijakazi wake anayemmiliki kwa mujibu wa Shari´ah, ni mamoja iwe kwa njia ya mateka au kwa kununua kwa watu waliothibitisha umiliki wao juu yake. Akimnunua na akasubiri hedhi moja, basi inajuzu kwake kumuingilia kama anavyofanya kwa mke wake. Ama mtumwa mwanaume, haruhusiwi kabisa kumuingilia bibi yake, kumbusu na wala kufanya jambo lolote la kimwili. Hii ni dhambi kwa makubaliano ya waislamu. Kazi yake ni kumtumikia tu kwa amri zake. Si lazima kwa bibi yake kujisitiri mbele yake. Lakini hata hivyo haina maana kuwa ni Mahram wake. Allaah amemruhusu kutojisitiri kwa sababu anapata uzito kutokana na wingi na kuingia na kutoka kwake, haina maana kuwa bibi huyo ni halali kwake. Kwa hivyo asimbusu, asimjamii na kadhalika. Hayo ni haramu kwake.
[1] 04:24
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3298/حكم-جماع-العبد-المملوك-لسيدته
- Imechapishwa: 04/10/2026
Swali: Je, kijakazi anaruhusiwa kwa bwana wake kumjamii, basi je, mtumwa mwanaume anaruhusiwa kumjamii bibi yake kwa idhini yake kutokana na maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ
”… isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume.”[1]
Jibu: Hapana, jambo hili ni maovu. Hili lililokuja katika Aayah linahusu wanaume, kama alivyosema (Ta´ala):
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
“Na ambao wanazihifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume basi hao hawalaumiwi.” (23:05-06)
Makusudio yake ni wajakazi kwa bwana wao. Ndiyo maana wametajwa pamoja na wake zao halali. Hivyo basi bwana anaruhusiwa kumuingilia mke wake wa ndoa na pia kijakazi wake anayemmiliki kwa mujibu wa Shari´ah, ni mamoja iwe kwa njia ya mateka au kwa kununua kwa watu waliothibitisha umiliki wao juu yake. Akimnunua na akasubiri hedhi moja, basi inajuzu kwake kumuingilia kama anavyofanya kwa mke wake. Ama mtumwa mwanaume, haruhusiwi kabisa kumuingilia bibi yake, kumbusu na wala kufanya jambo lolote la kimwili. Hii ni dhambi kwa makubaliano ya waislamu. Kazi yake ni kumtumikia tu kwa amri zake. Si lazima kwa bibi yake kujisitiri mbele yake. Lakini hata hivyo haina maana kuwa ni Mahram wake. Allaah amemruhusu kutojisitiri kwa sababu anapata uzito kutokana na wingi na kuingia na kutoka kwake, haina maana kuwa bibi huyo ni halali kwake. Kwa hivyo asimbusu, asimjamii na kadhalika. Hayo ni haramu kwake.
[1] 04:24
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3298/حكم-جماع-العبد-المملوك-لسيدته
Imechapishwa: 04/10/2026
https://firqatunnajia.com/mtumwa-mwanaume-kumjamii-bibi-yake/