Niache kumtembelea ndugu yangu anayependa kusengenya?

Swali: Nina ndugu yangu wa baba anaishi katika nyumba yake na ninapenda kumunga, lakini nikikaa naye huanza kuzungumzia huyu na kumsema vibaya yule katika jamaa kwa sababu ana matatizo ya kisaikolojia na anahusisha matatizo yake na watu hao anaowasema vibaya. Pamoja na kwamba ninajaribu kumuweka mbali na njia hiyo, lakini ang´ang´ania. Nifanye nini? Niachane na kumtembelea, nipunguze au nifanye nini?

Jibu: Mtembelee na umpe nasaha, umsaidie katika mambo ya dunia yake na dini yake kadiri ya uwezo wako. Usikate kumtembelea, kwani hiyo ni katika tabia ya watu; ni nani anayesalimika na usengenyi? Ni wachache sana. Watu wengi huzungumza kuhusu wengine: fulani amefanya hivi, fulani amesema hivi, fulani ana kasoro hii na ile. Lakini mpe nasaha na mwambie amche Allaah, kwamba haijuzu na Allaah ameliharamisha. Allaah amesema:

وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا

”Wala wasisengenyane baadhi yenu wengine.”[1]

Ilinde heshima ya ndugu zako katika kutokuwepo kwao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayemtetea ndugu yake katika kutokuwepo kwake, basi Allaah atamlinda uso wake na Moto siku ya Qiyaamah.”

Kwa hiyo jitahidi kutetea heshima za watu na umnasihi kwa maneno mazuri na mtindo mzuri. Huenda, kwa idhini ya Allaah, ukamwathiri kwa kurudiarudia. Hakika kitu kinaporudiwa mara kwa mara huacha athari. Hata kamba inapopita juu ya jiwe mara kwa mara huacha alama. Hivyo kurudia nasaha, kwa moyo mpana, maneno mazuri na njia nzuri, kwa idhini ya Allaah kutamwathiri na utapata ujira mkubwa.

[1] 79:12

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3313/حكم-قطع-زيارة-القريب-العاصي
  • Imechapishwa: 04/10/2026