Damu inayokuja katika zama za hedhi katika mtindo usiyo wa kawaida

Swali: Mwanamke amejiwa na wakati wa ada yake ya mwezi, lakini haikuwa kama kawaida yake. Bali damu ilikuwa ikimtoka kwa mfumo wa matone yaliyokatikakatika. Je, aache kuswali au hapana?

Jibu: Haizingatiwi kuwa ni hedhi, kwa sababu hedhi ni kutiririka kwa lugha. husemwa: Kwa hiyo tone na mfano wake havizingatiwi kuwa ni hedhi. Basi ajifunge pamba, atawadhe na aswali, hata ikiwa hilo litakuwa katika wakati wa ada yake. Kwa hiyo ikiwa katika wakati wa ada kuna siku za kukauka, basi ataswali. Kwa ajili hiyo wanazuoni wanasema kwamba mwenye kuona siku moja ya damu na siku moja ya kukauka, basi damu ni hedhi na kukauka ni twahara. Ikiwa ada yake ni siku sita, kisha akaona damu kwa siku tatu na akaona kukauka kwa siku moja, basi ataswali katika siku hiyo. Ikiwa damu itarudi katika wakati wa ada, basi atakaa na hataswali na kadhalika. Swalah yake ni sahihi katika siku ambayo kuna kukauka- Anazifanya siku za damu kuwa ni ada na siku za kukauka kuwa ni twahara, kama hedhi na twahara ya kawaida.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 04/10/2026