Bora swalah za Sunnah au Twawaaf?

Swali: Ni kipi bora zaidi katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhaan; kufanya Twawaaf kwenye Ka´bah au kuswali?

Jibu: Aina ya swalah ni bora zaidi, lakini mgeni aliyekuja kutoka mbali anapaswa kufanya Twawaaf kwenye Ka´bah kwa sababu ´ibaadah aina hii haipatikani katika mji wake. Swalah kwake ni katika aina ya Twawaaf. Nyakati ni pana. Katika wakati mmoja afanye Twawaaf na wakati mwingine aswali. Aidha azidishe kufanya Twawaaf kwenye Ka´bah ikiwa hakuna msongamano na wakati wa msongamano aswali.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 04/10/2026