Swali: Je, imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alimhimidi Allaah ndani ya swalah baada ya kupiga chafya?

Jibu: Silikumbuki hilo. Lakini Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) katika kisa cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kubaki nyuma na yeye kuwaswalisha watu kabla ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuja, aliinua mikono yake na akamhimidi Allaah. Kwa hiyo kumsifu Allaah ni Dhikr ambayo haipingani na swalah. Kwa hiyo ikiwa atamsifu Allaah ni Dhikr na haizingatiwi kuwa ni maneno.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 04/10/2026