Mtume anaswaliwa katika swalah ya kujitolea pia

Swali: Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni katika swalah ya faradhi au swalah zingine pia?

Jibu: Udhahiri wa Hadiyth mbalimbali ni ueneaji katika kila kitu. Baadhi ya mapokezi kwa Ibn Khuzaymah yanasema:

”Tukikuswalia katika swalah zetu… ”

Hapa tunapata faida kwamba ndani ya swalah kumetiliwa mkazo zaidi. Kwa ajili hiyo wakasema:

”Tumeshajua namna ya kukuswalia… ”

Ambako ni kule kusema:

السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume!”

Tamko jengine linasema:

”Ama salamu mmekwishajua… ”

Hili linaleta hisia kwamba ndani ya swalah kumetiliwa mkazo zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24295/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 24/09/2024