Mtu wa dini kusikiliza nyimbo na TV

Swali: Kuna wanaume wenye alama za wema, lakini wanafuatilia baadhi ya nyimbo na maigizo ya TV. Je, wana dhambi katika hilo?

Jibu: Kusikiliza nyimbo na maigizo yenye madhara yanayokwenda kinyume na Shari´ah, yanamdhuru kila mtu. Yanamdhuru anayeyasikiliza na anayeyaangalia. Ama akisikiliza mazungumzo ya kidini, Qur-aan na khabari muhimu, hilo halimdhuru.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1427/سماع-الاغاني-ومشاهدة-التمثيليات-التلفزيونية
  • Imechapishwa: 19/12/2025