Mtu anatakiwa kujitahidi kufanya ´ibaadah daima

Swali: Ni ipi tafsiri ya Aayah:

حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً

”Mpaka anapofikia umri wake wa kupevuka na akafikia miaka arobaini… ”[1]?

Je, ni sahihi yale yanayosemwa kwamba watu wa Madiynah mtu akifikisha miaka arobaini huwa anajitenga kwa ajili ya ´ibaadah?

Jibu: Aayah hii iko wazi katika maana yake. Ama kuhusu yale yanayosemwa juu ya watu wa Madiynah, mimi sina khabari kuhusu jambo hilo. Huenda baadhi ya watu walifanya hivyo, lakini sina uthibitisho wa hilo. Shari´ah inafahamisha ya kwamba muumini anatakiwa kufanya ‘ibaadah daima na ajitahidi katika kheri wakati wote, ni mamoja iwe ana miaka arobaini au sitini; na Aayah hii haipingani na hilo. Ndani ya Aayah kuna kuhimiza kumshukuru Allaah (Jalla wa ´Alaa), kumhimidi, kumsifu na kumuomba Allaah amruzuku kizazi chema. Hakuna ndani yake dalili ya kuacha kazi au shughuli. Bali ndani yake imo amri ya kufanya matendo:

وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ

”… na nipate kutenda mema Utakayoridhia.”[2]

[1] 46:15

[2] 46:15

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1102/الحث-على-العمل-والاجتهاد-في-العبادة-داىما
  • Imechapishwa: 25/01/2026