Mtu analipwa thawabu za matendo yake kabla ya kuritadi

Swali: Je, mtu analipwa thawabu za matendo yake kabla ya yeye kuritadi?

Jibu: Ndio:

”Umesilimu kwa matendo mema uliyoyafanya hapo awali.”

Ikiwa atasilimu na akanyooka sawasawa, basi Allaah atayahifadhi matendo yake yaliyotangulia.

Swali: Vipi ikiwa ataritadi kisha akasilimu?

Jibu: Matendo yake yaliyotangulia akiwa bado ni muislamu ni yake. Atahifadhiwa nayo. Kadhalika iwapo atasilimu matendo yake mema kabla ya kuja Uislamu.

Swali: Yeye amekutwa ni muislamu, lakini alinyoa ndevu zake au aliacha…

Jibu: Huko sio kuritadi, hayo ni maasi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29357/هل-يثاب-من-ارتد-ثم-اسلم-على-اعماله-السابقة
  • Imechapishwa: 11/07/2025