Mtu afanye nini ikiwa watu anaokaa naye nyumbani ni watenda madhambi?

Swali: Mtu afanye nini ikiwa marafiki zake anaokaa nao waovu ndio ndugu zake na wanaishi katika nyumba moja?

Jibu: Awalinganie kwa Allaah. Ikiwa wako na kitu katika maasi au shirki awalinganie kwa Allaah na awaelekeze. Wakikubaliwa ni sawa, vinginevyo jitenge nao mbali ili wasikuvute katika batili.

Swali: Ahame kutoka kwenye nyumba wanayoishi?

Jibu: Ikiwa unachelea juu ya nafsi yako wakuvute katika batili yao.

Swali: Hukumu ni hiyohiyo hata kama ni baba?

Jibu: Hukumu ni hiyohiyo hata kama ni baba.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24571/ما-يفعل-من-ابتلي-بجلساء-السوء-من-الاقارب
  • Imechapishwa: 03/11/2024